AFYA


Nimeona ni faida kubwa kwa wote kuweza kuwa na makala za afya, hivyo nitakua na kuandalia mfululizo wa makala maalumu chini ya blog hii ya

Kulinda uzima na usalama wa mwili ni miongoni mwa maudhui ambazo zimekuwa zikishughulisha fikra za mwanadamu katika kipindi chote cha uhai wa kiumbe hicho.

Woga wa maradhi na mauti daima ulimwandama mwanadamu. Kwa msingi huo alifanya jitihada za kushinda maradhi na magonjwa mbalimbali kwa msaada wa akili, elimu na uzoefu wake.
Katika njia hiyo ndefu, mwanadamu alipita katika vipindi na awamu tofauti. Kuanzia tiba ya kale na dawa za mitishamba hadi teknolojia na sayansi ya sasa, vyote vilitumiwa na mwanadamu katika juhudi zake za kutaka kuyashinda maradhi na mashaka yake.

Pamoja na hayo yote teknolojia isiyojua mipaka ya leo pia imemletea mwanadamu mashaka na matatizo mapya na kumfanya akabiliwe na aina mpya za magonjwa na maradhi.

Manyandahealthy