Kuhusu Sisi

MANYANDAHEALTHY
ManyandaHealty ni Mtandao wenye mjumuiko wa taarifa na makala mbalimbali zinazohusu Afya ya binadamu na Mazingira yake. Ambazo lengo lake ni kuhakikisha jamii ya kitanzania inafaidika na kupata habari na elimu juu ya maswala ya afya. lengo ni kuleta mwamko wa kufahamu umuhimu wa kuwa na afya bora kwa njia ya mawasiliano ya Mtandao, elimu,ushauri na mengineyo yahusuyo afya.

MANYANDAHEALTHY
Manyandahealthy.com ni Blog itakuwa ikijadili magonjwa na maradhi mbalimbali kwa kuangazia sababu zinazosababisha magonjwa hayo, dalili zake na hata matibabu na kinga za baadhi ya maradhi bila kusahau namna ya kupambana na maradhi hayo ili kuziimarisha afya zetu.

Katika Makala za Blog hii pia nitajitahidi kuwajulisha wasomaji wangu matokeo na tija za chunguzi na tafiti mbalimbali zinazohusiana na masuala ya afya na tiba hasa zile ambazo ni mpya au zimefanywa hivi karibuni. Vile vile makala afya katika blog hii hazitoacha kuwajulisha wasomaji wangu umuhimu wa vyakula mbalimbali kwa afya ya mwanaadamu.

Pia pale itakapowezekana tutakuwa tukiwasiliana mimi na wewe ukiuliza swali lako nami nitalifanyia kazi na pia kwa kuwashirikisha wataalamu zaidi wa tiba na madaktari mbalimbali ili kujibu maswali yenu mbalalimbali na masuala tofauti yanayohusu afya.
Ni matumaini yangu kuwa mtajumuika nasi na kufaidika na makala zangu katika blog yako ya www.manyandahealthy.com

Lengo likiwa ni kutuwezesha kuziimarisha afya zetu na kujikinga na maradhi mbalimbali sambamba na mazingira yake.

Tafadhalini msikose kuungana nami kila unapopata muda wa kuingia mtandaoni ili kufaidika na habari na makala mbalimbali zaidi kuhusu afya yako.


Afya Bora, Taifa Imara