
Kwa mujibu wa taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Tanzania ni kati ya nchi 10 duniani zinazochangia vifo vya watoto wachaga kwa
asilimia 66 duniani.
MAMA ANAWEZAJE KUJIKINGA ASIJIFUNGUE MTOTO NJITI?
Ingawa hakuna sababu ya moja kwa moja inayosababisha mjamzito
kujifungua mtoto njiti, lakini inatakiwa ajiepushe na kujikinga na tabia
hatarishi zinazoweza kusababisha tatizo hilo.

TABIA HATARISHI NI ZIPI?
Mama mtarajiwa anatakiwa ale vyakula bora hata kabla ya kubeba
ujauzito, kuacha kufanya hivyo kunasababisha baadaye mama huyu akibeba ujauzito
kujifungua mtoto njiti.
Pia, anatakiwa kuacha unywaji wa pombe kupindukia, uvutaji wa
sigara na matumizi ya dawa za kulevya.
Kuzarau kuanza kwenda kuliniki mapema baada ya kubeba ujauzito.
Mjamzito anapaswa kuanza kliniki mapema kwa ili apewe elimu juu
ya kulea mimba na kufanyiwa uchunguzi na kupimwa vipimo maalumu

Mjamzito hapaswi kulala bila chandarua kufanya hivyo kunamuweka
katika hatari ya kuugua malaria yanayoweza kumuathiri hata mtoto aliyeko
tumboni na kujikuta akijifungua kabla ya muda.
Mjamzito anapojifungua mtoto kabla ya kutimiza wiki 37, huyo
huitwa Njiti, anakua bado hajafikisha muda wake wa kuzaliwa na mwili wake
unakuwa bado haujakomaa.
NI DALILI ZIPI HUONYESHA MJAMZITO ATAJIFUNGUA MTOTO NJITI?
Ili kuepuka kuzaa mtoto njiti lazima mama ujue dalili zipi
ukiziona ama kujisikia unatakiwa uwahi hospitalini.
Moja ni maumivu ya mgonga yanayokuja na kuondoka na mara nyingi
maumivu hayo hutokea mara kwa mara maeneo ya chini ya mgongo.

Pili, maumivu kwenye sehemu za siri. Maumibu hayo huja kwa njia
kama ya kuvuta ukeni na kuachia kila baada ya dakika kumi. Kutokwa majimaji
mengi na damu inaweza kuwa kidogo ukeni, kuhara na kutapika, hizo ni miongoni
mwa dalili kuwa sasa mama huyo anaweza akajifungua kabla ya muda wake.
Dalili nyingine ni maumivu ya chini ya kitovu, mtoto kusukuma
kuja chini, kutokucheza kwa mtoto.
Mjamzito akibaini dalili hizo, anatakiwa awahi hospitali kwa sababu
mama ndiye anatakiwa kufuatilia mapigo ya mtoto tumboni, akisikia yupo kimya
ajaribu kunywa maji, uji, chai au kula chakula, kama yuko hai atacheza.
Hata hivyo, mtoto njiti mara nyingi huwa anakuwa katika hatari
kadhaa baada ya kuzaliwa, na baadhi ya hatari hizo ni pamoja tatizo katika
mfumo wa upumuaji.

Mara nyingi mapafu yake hushindwa kutanuka na kusinyaa wakati wa
upumuaji kutokana na kukosekana kwa protini maalumu mwilini mwake.
Hatari nyingine ni ya kupata maradhi ya kuambukizwa kirahisi na
anaweza pia kupata athari kwenye ubongo na matatizo ya mishipa, damu, mlango wa
fahamu na kuathirika kwa ogani.
Lakini pia mtoto huyu anakuwa kwe ye hatari ya kupata homa ya
manjano kutokana na ini kutokufanya kazi, uoni hafifu na huwa wanakuwa na
ukuaji mbaya.

KUMBUKA
Watoto hawa mara zote baada ya kuzaliwa huwa wanahifadhiwa
kwenye kifaa maalumu (incubator) kinachowapa joto la kutosha kama alilokua
analipata tumboni kwa mama.
Pia, kuna njia nyingine ya kuwahifadhi inayoitwa ‘Kangaroo’,
hapa mama au baba hutakiwa kumbeba mtoto huyo kifuani akiwa hana nguo, ila
huvishwa soksi na kofia na hufunikwa ili apate joto la kutosha. Ni njia moja
wapo ya kumpa joto linalo msaidia aishi na aweze kukua.
AINA ZA WATOTO NJITI
Watoto njiti wamegawanyika katika makundi, wapo wanaozaliwa
mimba ikiwa na wiki 28 na wapo wanaozaliwa mimba ikiwa na wiki kati ya 28 n 32.

Ila watoto wanaozaliwa mimba ikiwa na wiki 28 hadi 32 mara
nyingi hupata shida kwenye mfumo wa hewa na mapafu. Kundi la mwisho ni la
watoto wanaozaliwa wakiwa na wiki kati ya 32-37.
Na
Dk Ravinder Goodluck,