March 23, 2018

Jifunze Namna Ya Kuzungumza Na Daktari Wako


Related image
Kati ya makosa makubwa yanayofanywa na wagonjwa ni kutosema ukweli kwa watoa huduma wa afya. Sababu kubwa ya kutosema ukweli ni kujionea aibu. Mara nyingi wanaona wakisema ukweli kuhusiana na kitu kinachomsumbua ataadhirika.


Na mara nyingi hali hiyo hutokea kwa wagonjwa wengi wanaougua maradhi ya zinaa, akikutana na daktari ambaye ni tofauti na jinsia yake. Sababu nyingine inayowafanya wagonjwa wengi kutokuwa wazi kwa watoa huduma wa afya hasa kwa siku za karibuni ni tofauti ya umri kati ya mgonjwa na daktari. Mathalani inapotokea mgonjwa ana umri sawa au hata zaidi ya mzazi wa mtoa huduma hivyo mgonjwa anaona kama ni aibu kutoa siri zake za kiafya kwa mtoa huduma ambaye ana umri sawa na mtoto wake.
Image result for talk with doctor

Lakini mtu anapaswa kujua ukweli kuwa, kuficha tatizo kwa daktari ni hatari kwa kuwa tiba hutolewa kulingana na vipimo na vipimo huandikwa kutokana na maelezo ya mgonjwa.

Hivyo si jambo jema kuficha ukweli wa nini kikusumbuacho pale unapohojiwa na daktari au mtaalamu wa afya. Kwa mfano, wagonjwa wengi hukumbwa na aibu kusema kwa daktari kuwa alikunywa pombe muda mfupi kabla ya kufika hospitali kwa ajili ya matibabu ya dharura. Wakati unafikiria kumdanganya mtoa huduma wako wa afya unapaswa pia kufikiria madhara yatakayokupata kutokana na kuzungumza uongo.
 Related image
Kwa sababu daktari atalazimika kukufanyia vipimo tofauti na tatizo linalokusumbua. Hivyo ni vyema kuwa muwazi kwakuwa itamsaidia daktari aanze na huduma ya kuondoa kiasi cha pombe kilichomo mwilini, ili utakapofanyiwa vipimo, upate majibu sahihi kuhusu tatizo lako. Mwingine utakuta ni mvutaji wa sigara, lakini akiulizwa anasema havuti.

Lakini ikumbukwe kuna baadhi ya tiba hasa ya vidonge inaharibiwa na utendaji kazi wake mwilini na ile sumu inayopatikana kwenye moshi wa tumbaku ambayo kitaalamu inaitwa ‘Nicotine’. Kwa mfano mtu anakohoa mara kwa mara au anapungua uzito kwa kasi na anajisikia maumivu makali ya kifua. Ni vyema akamwambia daktari kua pamoja na maumivu hayo, lakini pia anavuta sigara.
Kwa kufanya hivyo utamsaidia daktari pampja na kutibu maradhi hayo mengine, anaweza kukupa tiba ya kuacha kuvuta sigara haraka iwezekanavyo kwa kuwa uvutaji wa sigara ni hatari sana kwa afya.
 Image result for talk with doctor
Wagonjwa wengi huwa wagumu kukiri pale anapobainika anaugua maradhi ya zinaa nay a afya ya uzazi. Sababu kubwa ni aibu. Wengi hujikuta wanaugua maradhi ya zinaa kutokana na tabia ya kufanya ngono isiyo salama na mbaya zaidi hufanya ngono na washirika tofauti tofauti ndani ya kipindi kifupi. Wagonjwa wengi huwa wazito kuwa wawazi kwenye eneo hio na wakijitahidi kusema ukweli, atakuambia “nilifanya ngono na mshirika mmoja tu mwaka huu.” Tukumbuke kuwa daktari hayupo kwa ajili ya kukuhukumu ila yupo kwa ajili ya kukusaidia.
 Image result for talk with doctor
Hivyo kuwa muwazi kwa kumueleza idadi ya watu ulioshirikiana nao tendo la ndoa kwa muda husika, kutamsaidia kukupatia msaada wa huduma ya maradhi ya zinaa na afya ya uzazi. Kama una gonjwa lolote la zinaa basi unapaswa kukubaliana na ukweli kubwa unaumwa ugonjwa wa zinaa. Lakini hata kama ulikuwa na gonjwa la zinaa hapo awali, daktari pia anapaswa kujua hilo.

Unaweza ukaona aibu kulisema hilo, lakini unapswa kujua ukweli kuwa baadhi ya magonjwa ya zinaa yanaweza kuwa hatari kama hayakupatiwa tiba stahiki. Pia ni vyema kufahamu kuwa hata kama ulishawahi kuwa na ugonjwa wowote wa zinaa na baada ya muda ukatoweka, upo hatarini kujirudia bila kutibiwa.
Unaporudi unakuwa na hatari zaidi kwa afya ikiwemo hata kusababisha kupoteza uwezo wa kuzaa.

Kukabiliana na aibu ukiwa na daktari wako kutakusaidia kuepukana na aibu utakazokutana nazo hapo baadaye kwenye maisha yako.
Eneo lingine ambalo wagonjwa wengi wanakuwa wagumu kusema ukweli ni tatizo la nguvu za jinsia.
 Related image
Kukosa nguvu za jinsia ni tatizo linaloathiri jinsia zote mbili. Japo imezoeleka kwa wanaume zaidi lakini huwatokea pia hata wanawake wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Hivyo ni vyema kumjulisha daktari bila kuona aibu kama tatizo hilo unalo.
Kwa kufanya hivyo kutamsaidia daktari kukupa tiba ya uhakika inayoendana na dalili zako au kukupa msaada wa kisaikolojia.

Na Dk Christopher Peterson


Share: