August 3, 2016

Kipimo Cha Mimba Cha Nyumbani

Image result for upt test

Kipimo cha mimba cha nyumbani ni rahisi sana kukitumia wewe mwenyewe kwa wakati wako ikiwa unajihisi umjamzito au kuhisi mwenzi wako ana ujauzito.
Unachotakiwa kuwa nacho ni moja, Kipimo hichob‘Pregnancy Test’ ambacho kinapatikana katika maduka yote ya madawa ya Binadamu, na pili mkojo wa anahisiwa au kuhisi ana mimba.

mara nyingi ni rahisi zaidi kupata majibu ya uhakika ukitumia mkojo wa kwanza kabisa asubuhi kisha uweka kwenye kikopo kidogo na kisha fuata maelekezo ya kwenye picha hii:-
Image result for upt test
Hatua;
1.   Fungua pakiti iliyo na kipimo cha mimba.

2.   Tofautisha sehemu ya kushika na sehemu utakayotumbukiza kwenye kikopo chenye mkojo.

3.   Acha kwa dakika zipatazo 3, bila kuzidisha sehemu yenye mstari uliyoandikwa MAX.

4.    Toa na kisha soma majibu yaliotokea.
Majibu yatatoka kama ilivyo katika picha hii inayofuata ya vipimo viwili tofauti vilivyofanyiwa majaribio:-

1.   Mistari miwili humaanisha ‘POSTIVE’ – Mimba imetunga.

2.   Mistari mmoja humaanisha ‘NEGATIVE’ – Mimba haikutunga.
 
Muonekano wa nje wa Kipimo cha Mimba kwa kutumia mkojo kinachopatikana kwa wingi katika maduka ya madawa mengi.
Ikiwa hujaamini matokeo yaliyotoka unashauriwa uende Hospitali kwa majibu kamili na sahihi kutoka kwa Daktari.


Share: