November 30, 2014

Rushwa katika huduma za afya

Unapofika kutibiwa katika hospitali hizi
kama huna pesa ya kutoa ‘kitu kidogo’, basi
tatizo la kuweza kumalizwa ndani ya siku
moja linaweza kukuchukua hadi mwezi
kutokana na nenda rudi utakayokutana
nayo.
Share:

Madhara ya kujichubua/ kuji cream.

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,
Share:

Kukabiliana na upungufu wa nguvu za kiume

Upungufu wa nguvu za kiuume wengi hapa duniani
huamini kuwa, mwanaume hasa ni
yule anayeweza kufanya tendo
hilo kwa muda mrefu na mara
nyingi ndio maana vijana wengi
utawasikia wakijisifu kuwa,
Share:

Faida za kunywa Maziwa mtindi

Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.
Share:

Umuhimu wa ndizi mbivu katika afya yako

Baada ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuiangalia ndizi kwa mtazamo tofauti na uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili.

Share:

Vyakula 10 vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili.
Share:

Mambo muhimu za kuzuia na kupunguza chunusi

Chunusi ni tatizo sugu linalosababishw a na

mambo kadha wa kadha. Tafiti nyingi za kisayansi zimeshafanywa na zinaendelea
mpaka leo kutafuta mbinu au tiba ya haraka kwa tatizo hili.

Kimila, wengi husema chunusi ni dalili ya kutunikiwa kupendwa na mtu aliyeko mbali na usiyemfahamu (secret admirer), eti basi
ndio maana unatokwa na chunusi (tabasamu basi kidogo). Wapo wanaosema zipo chunusi
za kupevusha yai la hedhi kwa wanawake na wasichana pindi tarehe za mzunguko wake
zinapokaribia. 

Chunusi za namna hii humtoka
mtu kamoja tu na kuwa haijifichi kabisa huku
chache huwatoka katika masikio na wengine
ndani ya pua.

Matokeo ya tafiti za kisayansi za kiutaalam
imegundua kwamba chunusi husababishwa
na kuongezeka kwa uzalishwaji wa
'Testosterone hormone' na mafuta ya mwili
'sebum' wakati wa mabadiliko ya kimwili

(Sebum ni aina ya mafuta kama nta yanayozaliwa kwenye vinyweleo chini ya
ngozi yako). Chunusi pia husababishwa na
msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia
pamoja na lishe iliyojaa sukari nyingi na
mafuta. 

Bidhaa kama Manjano (Turmeric),
giligilani, nyanya, ndimu, Aloe Vera, Zinc na
Vitamin ‘A’ ni vitu vya asili vinavyo weza kutibu chunusi. Kuna baadhi ya bidhaa ambazo hazishauriwi kutumiwa hasa kama
mtu unatatizo la kiafya au mjamzito hivyo unatakiwa kuwasiliana na daktari wako kwa
ushauri kabla ya kutumia hizi vitamin nadawa.

T1PS MUHIMU ZA KUZINGATIA
1. Hakikisha unaacha kama sio unapunguza
vyakula vyenye mafuta sheteshete na sukari
nyingi mpaka utakapomaliza tiba yako. Mfano
chipsi, vitumbua, chapati, keki, biskuti, pipi,
soda, nk uviache au upunguze mpaka
utakapopona chunusi.

2. Umeshasikia mara nyingi kuwa “maji ni
tiba”, jenga tabia ya kunywa maji angalau
glasi 8 kwa kutwa nzima

3. Osha uso wako mara mbili kwa siku.
Usinawe uso wako mara kwa mara kama
samaki. Tumia sabuni iliyoandikwa ‘mild
soap’ (mfano Protex Acne Soap au gentle
facial wash) na maji ya vuguvugu wakati wa
kuosha uso wako.

4. Tumia cream au lotion yenye ‘benzoyl
peroxide’ ndani yake. Ukienda pharmacy
(duka la dawa) unaweza kuulizia kwa
muhudumu.

5. Usijaribu kuzitumbua chunusi mwenyewe
maana unaweza kusukuma ‘infection’
ikaingia zaidi ndani ya ngozi yako ambayo
itasababisha uvimbe mwingine na wekundu
kujitokeza. Kama unataka kuzitumbua
chunusi zilizoiva ni vyema uende ‘Professional
salon’ ukafanyiwe ‘facial treatment’ kitaalam.

6. Kama unahitaji kuondoa chunusi kwa ajili
ya shughuli maalum kama harusi au mkutano
ukiwa kama mtoa mada, nenda kwa daktari
wa ngozi ‘dermatologist’ akusaidie
kukupatia tiba ya chapchap. Maana anaweza
kukuandikia dawa za antibiotics za kumeza
au za kupaka – itategemea na hali ya chunusi
na ngozi yako.

7. Jaribu kujizuia kugusa uso wako na
mikono kila mara. Ukiwa unaongea kwenye
simu jaribu kuzuia simu isiguse uso wako –
kunaweza kukawa na ‘sebum’ juu ya ngozi
yako itakayokuathiri .

8. Hakikisha unanawa mikono yako mara kwa
mara kila unapotoka chooni au kila baada ya
masaa kadhaa. Unaweza pia kutumia
‘antibacterial hand gel’. Mikono yako mara
zote iwe misafi.

9. Unapotaka kugusa uso wako mara zote,
hakikisha umenawa mikono yako na sabuni
hasa kabla ya kupaka lotion, cream au make-
up.

10. Kama una vaa miwani, inatakiwa
zipanguswe mara kwa mara maana zinaweza
zoa 'sebum' kwenye ngozi yako.

11. Ngozi yako intakiwa ipumue. Kama
chunusi ziko mgongoni, kwenye mabega au
kifuani, hakikisha unavaa nguo zisizobana.
Kama inakubidi kuvaa nguo za kubana
hakikisha ni safi na unazifua mara kwa mara.

12. Usiende kulala na make-up usoni. Tumia
make-up isiyokuwa na mafuta au soma label
iliyoadikwa ‘Oil free’.

13. Nywele zako zinazogusa usoni ziwe safi
wakati wote au zisiguse uso wako kabisa
maana na zenyewe pia zina uwezo wa kuzoa
‘sebum’ na kuambukiza sehemu zingine
ambazo chunusi hazijatokea.

14. Epuka na jua kali maana mionzi mingi ya
jua kwenye uso au ngozi yako huleta jasho na
kuzalisha ‘sebum’.

15. Hakikisha foronya ya mto wako
unabadilisha kila baada ya siku moja au mbili.
Inashauriwa kama una chunusi zifuliwe kila
siku - hasa kama usiku unatokwa na jasho
usoni wakati wa kulala. Kuna uwezekano
mkubwa wa ‘sebum’ kubakia kwenye foronya
na kuambukiza sehemu zingine za ngozi yako.


manyandahealthy@gmail.com

Share:

Matatizo ya kiafya yatokanayo na kazi

SHUGHULI za kila siku ofisini,
ziwe za kuajiriwa ama za
kujiajiri huweza kuwa sababu ya
matatizo fulani ya kiafya kwa
watu. Baadhi ya matatizo haya
ni madogo ama huonekana
madogo lakini huweza kukua na
kuwa makubwa kutokana na
kujirudia rudia hadi kumletea
mtu matatizo makubwa katika
maisha.
Share:

Si kila Homa Na maumivu ya kichwa ni malaria

Kujibashiria kuwa una Malaria wakati huna, kupata vipimo visivyo sahihi ni miongoni mwa mambo yanayochangia usugu wa maradhi hayo. Watanzania wengi wamejenga tabia ya kunywa dawa za Malaria bila kupima afya zao na huku wakikosa huduma sahihi hali ambayo inaelezwa kuchangia kuenea kwa vimelea vya ugonjwa huo na kusababisha usugu wa dawa.

Share:

Hatari ya malaria kwa mama mjamzito


Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani katika kupambana na ugonjwa wa malaria pia kuhamasisha uelewa ili kukabiliana na ugonjwa huu unaoongoza kwa kuua watu wengi.
Wataalamu wa afya wanaelezea uogonjwa wa malaria kuwa ni tishio kwa mama mjamzito na mtoto aliye bado kuzaliwa.
Share:

Maumivu ya korodani (testicular pains)KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodani ili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa. Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali.
Share:

Madhara ya kunywa maji baridi:

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku.
Share:

Jinsi ya tunza afya yako

Kutunza afya yako kunaweza kuboresha utendaji wako shuleni, kazini na pia kuboresha maisha yako.
NI JAMBO linalopatana na akili kutunza mwili ambao Mungu alikupa. Kwa mfano: Wazia kwamba una gari, lakini hulitunzi. Muda si muda, gari hilo litaharibika. Jambo hilohilo linaweza kutukia kwa mwili wako.
Share:

Tiba ya Juisi ya nyanya

Wengi wetu tunaifahamu nyanya kama kiungo kwenye mapishi yetu au hata kachumbari kwenye mlo.
        Hata hivyo, watafiti nchini marekani wamebaini kuwa wanawake wanaokunywa juisi ya nyanya angalau mara moja kwa wiki,
Share:

Magonjwa yanayosababishwa na maziwa


Ugonjwa huu utokanao na kunywa maziwa huwapata watu fulani wanapotumia maziwa na bidhaa za maziwa.SAA moja hivi imepita tangu ulipomaliza kula aiskrimu au jibini unayopenda sana. Tumbo lako limefura, linasokota, na lina gesi.
Share:

Mazoezi ya kupunguza maumivu

Maumivu ya nyonga huweza kuandamana naya kiuno, nyonga huunganisha miguu na mifupa ya mapaja inayotengeneza kiuno. Nyonga ndiyo inayofanya utembee kutoka sehemu moja hadi nyingine,
Share:

November 27, 2014

Jinsi ya kulinda ngozi yako!


“Watu hawatambui hatari kubwa inayosababishwa na jua. na jinsi linavyoweza kudhuru chembe za urithi za ngozi. Madhara ya muda mrefu yanaweza kutokeza kansa ya ngozi baadaye.
Share:

November 24, 2014

Matibabu ya utando mdomoni


Ugonjwa huu wa utando mdomoni Mgonjwa anapopata homa kali ikiambatana na kutetemeka kwa mwili na akishindwa kabisa kumeza basi apelekwe hospitali haraka iwezekanavyo ili aweze kuoatiwa matibabu.
Share:

November 21, 2014

November 19, 2014

Dalili, Ishara, za mjamzito kujifungua


Tuliona kuwa kipindi cha kujifunga hutabiriwa lakini siku rasmi mara nyingi haitabiriki. Wengi hufikiria kuwa dalili ya kwanza ya kutaka kujifungua ni kupasuka kwa chupa. Hii si sahihi, chupa inaweza isipasuke hadi hadi hatua za mwisho.
Share:

November 14, 2014

Nyakati tofauti za kujifungua mtoto

Katika makala zilizopita mengi yaliongelewa kuhusu ujauzito na umuhimu wa mahudhurio ya kliniki. Jambo hili ni sehemu tu ya kile kinachopaswa kufanywa ili uzazi uhesabike kuwa salama.
Share:

November 13, 2014

Jinsi ya kujikinga na Virusi Vya Ebola

1. EBOLA NI NINI?
Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kitaalam (Ebola Virus). Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za virusi zinazosababisha kutoka damu mwilini.
Share:

Maradhi ya ngozi kwa njia ya ngono/ warts

Baadhi ya maswali tuliyopokea, mengi yalihusu maradhi ya sunzua ambayo kitaalmu yanajulikana kama warts.  Sunzua ni ugonjwa wa ngozi unaofahamika na wengi. Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo kitaalamu huitwa human papilloma virus.
Share:

November 12, 2014

Chanzo cha kikohozi kwa watoto

Kukohoa ni kiashiria kinachojitokeza pale mapafu yanapojihami dhisi ya takataka au mrundikano wa majimaji au ute ndani ya mapafu na mfumo wa juu wa hewa.
Share:

November 11, 2014

Ugonjwa wa mafindofindo

Kumekuwa na uelewa mdogo wa suala la vidonda vya koo maarufu kama mafindofindo katika jamii zetu. Watu wengi wamekuwa wakiamini uognjwa huu unasababishwa na utumiaji wa vitu vya baridi kama vile ice cream na barafu.
Share:

November 10, 2014

Tatizo la kukoroma

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene.
Share:

Tatizo la Kichefuchefu kwa wanawake zaidi

 
Watu wengi wanaume kwa wanawake, husumbuliwa na matatizo ya ulaji yanayoathiri afya na mfumo wa maisha yao ya kila siku.
Moja ya matatizo yanayohusiana na ulaji ni tatizo la muda mrefu la kichefuchefu,
Share: