Breaking News

December 24, 2014

chanzo na Dalili, kinga na tiba ya tatizo la KIPANDAUSO

Kichwa huuma kwa kupigapiga upande mmoja tu. Huenda mgonjwa akahisi pia kichefuchefu na asiweze kustahimili mwangaza mwangavu. Maumivu hayo yanaweza kuchukua saa chache au hata siku kadhaa.

Dalili, kinga na tiba ya Tatizo la Kukosa Choo

Kukosa choo kwa siku moja kitaalamu,  siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kutajwa kuwa na tatizo hilo iwapo atakosa choo kwa angalau zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.

Faida za Pilipili Hoho kiafya

Pilipili hoho Iwe za njano, nyekundu ama kijani, pilipili hoho zinatajwa kuwa mboga yenye vitamin zaidi ya 30. Kila vitamin ina kazi yake katika mwili wa binadamu lakini kubwa zaidi ni pale,

Sababu za vidonda mdomoni kwa watoto

Mdomoni ni eneo ambalo limeundwa na mishipa ya fahamu ya kutosha ndio maana uwepo wa vidonda mdomoni huambatana na maumivu makali.

December 23, 2014

Mazoezi kwa wenye ugonjwa wa kisukari

Watu wenye kisukari wanahamasishwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweka kiwango cha chao cha sukari, pia kujiondoa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo.

December 16, 2014

Ugonjwa wa Fizi

UGONJWA wa Fizi unawapata watu wengi sana ulimwenguni. Hata hivyo, katika hatua za kwanza dalili zake hazionekani haraka. Ugonjwa wa fizi ni hatari kwa kuwa hautambuliki mapema.

December 14, 2014

Ugonjwa wa Fistula na matibabu yake

Kwa lugha ya kitalaamu ugonjwa huu hujulikana kama Peri-anal fistula au (Fistula in ano). Ni tatizo la kuwapo kwa tundu au matundu karibu na njia ya haja kubwa.

Faida Za Kula Tikikiti Maji Kiafya


Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.

December 12, 2014

Faida ya Bamia kwa wenye vidonda vya tumbo

Unafahamu kuwa kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali kama vidonda vya tumbo

December 4, 2014

Ugonjwa wa pumu (asthma) na matibabu yake

PUMU /asthma ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingia na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa huvimba na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na kutoka kwenye mapafu.

Tiba ya kuondoa sumu, Vidonda na Kuongeza Nguvu


Ni uti wa mgongo na bidhaa ya kwanza kutengenezwa na kampuni. Inatokana na gel la katikati la jani la aloevera.

December 2, 2014

Ugonjwa wa Saratani ya tezi dume

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu.

Jinsi ya kuzuia mafua kwa watoto

Mafua ni moja ya magonjwa ya mfumo wa hewa ambayo mara kwa mara huwapata watoto wa chini mitano. Mafua huweza kuwapa watoto mara 5-10 kwa mwaka mmoja.

December 1, 2014

Jinsi ya kudumisha uzito wa kawaida wenye afyaKudumisha uzito wa mwili bora unakusaidia wewe kutokana na hatari
Unapaswa kufahamu ya kwamba unakula zaidi kama unazindisha kulingana na vile mwili wako unavyohitaji.

Lishe bora kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwiWatu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
wamekuwa wakitafuta taarifa zaidi kuhusu
ulaji wa vyakula mbalimbali siku hadi siku.
Baadhi ya taarifa wanazozipata,

Ukimwi na kifua kikuu magonjwa yanayokwenda sambamba


Asilimia kubwa ya watu wanaougua
ugonjwa wa kifua kikuu (TB) duniani
wamekuwa wakigundulika pia kuwa na
Virusi Vya Ukimwi(VVU).

Umuhimu wa calcium na magnesium kwa mama mjamzito

Umuhimu wa Calcium na Magnesium kwa
mama Mjamzito na anayenyonyesha
Mama mjamzito au anayenyonyesha
anahitaji 1600 hadi 2000 mg za calcium kila
siku. 

Shinikizo la damu la juu (hypertension)

Shinikizo la damu la juu (Hypertension) au
presha ya damu ya juu (High Blood
Pressure), pia huitwa shinikizo la mishipa
(Arterial Hypertension) ni hali ya ugonjwa

Jinsi ya kuishi na vidonda vya tumbo

Kama una vidonda vya tumbo, matibabu
yako yatategemea sababu ya vidonda vya
tumbo. Kama ni bakteria H.pylori, dawa za
kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Faida 12 za machungwa

Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.

November 30, 2014

Rushwa katika huduma za afya

Unapofika kutibiwa katika hospitali hizi
kama huna pesa ya kutoa ‘kitu kidogo’, basi
tatizo la kuweza kumalizwa ndani ya siku
moja linaweza kukuchukua hadi mwezi
kutokana na nenda rudi utakayokutana
nayo.

Madhara ya kujichubua/ kuji cream.

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,

Kukabiliana na upungufu wa nguvu za kiume

Upungufu wa nguvu za kiuume wengi hapa duniani
huamini kuwa, mwanaume hasa ni
yule anayeweza kufanya tendo
hilo kwa muda mrefu na mara
nyingi ndio maana vijana wengi
utawasikia wakijisifu kuwa,

Faida za kunywa Maziwa mtindi

Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Umuhimu wa ndizi mbivu katika afya yako

Baada ya kusoma makala yangu ya leo na kuzingatia nilichokiandika, bila shaka utaanza kuiangalia ndizi kwa mtazamo tofauti na uliokuwa nao hapo awali. Ndizi mbivu ni tunda maarufu sana duniani lakini ni watu wachache wanaojua uwezo, faida na maajabu yaliyomo kwenye tunda hili.

Vyakula 10 vinavyoongeza uwezo katika tendo la ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili.

Mambo muhimu za kuzuia na kupunguza chunusi

Chunusi ni tatizo sugu linalosababishw a na

mambo kadha wa kadha. Tafiti nyingi za kisayansi zimeshafanywa na zinaendelea
mpaka leo kutafuta mbinu au tiba ya haraka kwa tatizo hili.

Kimila, wengi husema chunusi ni dalili ya kutunikiwa kupendwa na mtu aliyeko mbali na usiyemfahamu (secret admirer), eti basi
ndio maana unatokwa na chunusi (tabasamu basi kidogo). Wapo wanaosema zipo chunusi
za kupevusha yai la hedhi kwa wanawake na wasichana pindi tarehe za mzunguko wake
zinapokaribia. 

Chunusi za namna hii humtoka
mtu kamoja tu na kuwa haijifichi kabisa huku
chache huwatoka katika masikio na wengine
ndani ya pua.

Matokeo ya tafiti za kisayansi za kiutaalam
imegundua kwamba chunusi husababishwa
na kuongezeka kwa uzalishwaji wa
'Testosterone hormone' na mafuta ya mwili
'sebum' wakati wa mabadiliko ya kimwili

(Sebum ni aina ya mafuta kama nta yanayozaliwa kwenye vinyweleo chini ya
ngozi yako). Chunusi pia husababishwa na
msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia
pamoja na lishe iliyojaa sukari nyingi na
mafuta. 

Bidhaa kama Manjano (Turmeric),
giligilani, nyanya, ndimu, Aloe Vera, Zinc na
Vitamin ‘A’ ni vitu vya asili vinavyo weza kutibu chunusi. Kuna baadhi ya bidhaa ambazo hazishauriwi kutumiwa hasa kama
mtu unatatizo la kiafya au mjamzito hivyo unatakiwa kuwasiliana na daktari wako kwa
ushauri kabla ya kutumia hizi vitamin nadawa.

T1PS MUHIMU ZA KUZINGATIA
1. Hakikisha unaacha kama sio unapunguza
vyakula vyenye mafuta sheteshete na sukari
nyingi mpaka utakapomaliza tiba yako. Mfano
chipsi, vitumbua, chapati, keki, biskuti, pipi,
soda, nk uviache au upunguze mpaka
utakapopona chunusi.

2. Umeshasikia mara nyingi kuwa “maji ni
tiba”, jenga tabia ya kunywa maji angalau
glasi 8 kwa kutwa nzima

3. Osha uso wako mara mbili kwa siku.
Usinawe uso wako mara kwa mara kama
samaki. Tumia sabuni iliyoandikwa ‘mild
soap’ (mfano Protex Acne Soap au gentle
facial wash) na maji ya vuguvugu wakati wa
kuosha uso wako.

4. Tumia cream au lotion yenye ‘benzoyl
peroxide’ ndani yake. Ukienda pharmacy
(duka la dawa) unaweza kuulizia kwa
muhudumu.

5. Usijaribu kuzitumbua chunusi mwenyewe
maana unaweza kusukuma ‘infection’
ikaingia zaidi ndani ya ngozi yako ambayo
itasababisha uvimbe mwingine na wekundu
kujitokeza. Kama unataka kuzitumbua
chunusi zilizoiva ni vyema uende ‘Professional
salon’ ukafanyiwe ‘facial treatment’ kitaalam.

6. Kama unahitaji kuondoa chunusi kwa ajili
ya shughuli maalum kama harusi au mkutano
ukiwa kama mtoa mada, nenda kwa daktari
wa ngozi ‘dermatologist’ akusaidie
kukupatia tiba ya chapchap. Maana anaweza
kukuandikia dawa za antibiotics za kumeza
au za kupaka – itategemea na hali ya chunusi
na ngozi yako.

7. Jaribu kujizuia kugusa uso wako na
mikono kila mara. Ukiwa unaongea kwenye
simu jaribu kuzuia simu isiguse uso wako –
kunaweza kukawa na ‘sebum’ juu ya ngozi
yako itakayokuathiri .

8. Hakikisha unanawa mikono yako mara kwa
mara kila unapotoka chooni au kila baada ya
masaa kadhaa. Unaweza pia kutumia
‘antibacterial hand gel’. Mikono yako mara
zote iwe misafi.

9. Unapotaka kugusa uso wako mara zote,
hakikisha umenawa mikono yako na sabuni
hasa kabla ya kupaka lotion, cream au make-
up.

10. Kama una vaa miwani, inatakiwa
zipanguswe mara kwa mara maana zinaweza
zoa 'sebum' kwenye ngozi yako.

11. Ngozi yako intakiwa ipumue. Kama
chunusi ziko mgongoni, kwenye mabega au
kifuani, hakikisha unavaa nguo zisizobana.
Kama inakubidi kuvaa nguo za kubana
hakikisha ni safi na unazifua mara kwa mara.

12. Usiende kulala na make-up usoni. Tumia
make-up isiyokuwa na mafuta au soma label
iliyoadikwa ‘Oil free’.

13. Nywele zako zinazogusa usoni ziwe safi
wakati wote au zisiguse uso wako kabisa
maana na zenyewe pia zina uwezo wa kuzoa
‘sebum’ na kuambukiza sehemu zingine
ambazo chunusi hazijatokea.

14. Epuka na jua kali maana mionzi mingi ya
jua kwenye uso au ngozi yako huleta jasho na
kuzalisha ‘sebum’.

15. Hakikisha foronya ya mto wako
unabadilisha kila baada ya siku moja au mbili.
Inashauriwa kama una chunusi zifuliwe kila
siku - hasa kama usiku unatokwa na jasho
usoni wakati wa kulala. Kuna uwezekano
mkubwa wa ‘sebum’ kubakia kwenye foronya
na kuambukiza sehemu zingine za ngozi yako.


manyandahealthy@gmail.com

Mjamzito kumwambukiza VVU mtoto aliye tumboni

Swali: Mimi ni mjamzito, je kama
nimeambukizwa VVU mtoto aliye
tumboni anapataje VVU? na je kama
anapata kuna njia ya kuweza
kusaidia nijifungue bila VVU?

Aina mbili za VVU Nchini kwetu Tanzania

Swali: Je, ni kweli kuna aina mbili
za VVU? Kama ndivyo hapa nchini
kwetu ipi ina idadi kubwa ya
kuambukiza?

Watu wengine wana VVU lakini hawapati ukimwi

Swali: Ni kwa nini watu wengine
wana VVU lakini hawapati Ukimwi?

Mashine za kunyolea saluni zinaambukiza VVU?

Swali: Je mashine za kunyolea
saluni zinaambukiza VVU?

Kunawa na sabuni baada ya kujaamiiana na mtu mwenye VVU hakuui VVU

Swali: Je, kunawa na sabuni baada
ya kujaamiiana na mwanamke
mwenye VVU kunaua VVU?

Kunyonyana ulimi au kula mate Kunasababisha kuambukiza VVU?

Swali: Je kunyonyana ulimi au kula
mate kunaweza kuambukiza VVU?

Si kweli kila anaegua TB ana VVU?

Swali : Je ni kweli kila anaegua TB
ana VVU?

Mwanaume asiyetahiriwa hupatwa VVU kwa urahisi

Swali: Ni kweli mtu asiyetahiriwa
hupatwa VVU kwa urahisi?

Jibu: Ni kweli mtu asiyetahiriwa
ana asilimia 60 zaidi ya kupata VVU

Vifaa vya kung’olea meno vinachangia maambukizi ya VVU?

Swali: Vipi kuhusu vifaa vya
kung’olea meno vinachangia
maambukizi ya VVU? Maana huwa
havitupwi alivyotumia mwenzako
kesho na wewe hivyo hivyo.

Mtu mwenye VVU Anaweza kupewa dawa za kuzuia Asipate maambukizi YA VVU.

Swali: Kama jana nilijamiiana na
mtu mwenye VVU naweza kupewa
dawa za kuzuia nisipate
maambukizi?

Dawa za ARVs zina athari na unywaji wa pombe

Swali: Je, Dawa Za Arvs Zina Athari
Na Unywaji Wa Pombe?

Madhara ya Sabuni za kurudisha ubikira!!!

WANAWAKE wameshauriwa
kuacha kutumia sabuni za
kunawia sehemu za siri ambazo
hudaiwa kurejesha ubikira
kwani zina madhara makubwa
ikiwemo kusababisha kansa ya
shingo ya kizazi.

Matatizo ya kiafya yatokanayo na kazi

SHUGHULI za kila siku ofisini,
ziwe za kuajiriwa ama za
kujiajiri huweza kuwa sababu ya
matatizo fulani ya kiafya kwa
watu. Baadhi ya matatizo haya
ni madogo ama huonekana
madogo lakini huweza kukua na
kuwa makubwa kutokana na
kujirudia rudia hadi kumletea
mtu matatizo makubwa katika
maisha.

Sababu za kupoteza hamu ya kujamiiana

 kusababisha msisimko
kupotea kati ya wenza wawili na
hatimaye mwisho ni kupungua
uwezo au hamu ya kujamiana.

Madhara ya Unene na shida ya matibabu

Unene(obesity), ni ugonjwa unaokua kwa
kasi kipindi hiki ukiambatana na madhara
makubwa kiafya hata vifo.
Unene hupimwa kwa kutumia kipimo

Madhara ya usafiri na misongamano ya watu vichocheo vya magonjwa


Ni wazi kuwa wengi wanatumia usafiri wa
umma kwa sababu ya uwezo, lakini unayo
madhara yake mengi kwa afya zao
Asubuhi inapofika, aghalabu asilimia 80 ya
Watanzania huongoza njia kutafuta usafiri

Si kila Homa Na maumivu ya kichwa ni malaria

Kujibashiria kuwa una Malaria wakati huna, kupata vipimo visivyo sahihi ni miongoni mwa mambo yanayochangia usugu wa maradhi hayo.

Watanzania wengi wamejenga tabia ya kunywa dawa za Malaria bila kupima afya z

VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (pmtct)Kwa kawaida, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) yanaweza kutokea kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Hatari ya malaria kwa mama mjamzito


Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani katika kupambana na ugonjwa wa malaria pia kuhamasisha uelewa ili kukabiliana na ugonjwa huu unaoongoza kwa kuua watu wengi.
Wataalamu wa afya wanaelezea uogonjwa wa malaria kuwa ni tishio kwa mama mjamzito na mtoto aliye bado kuzaliwa.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kujifungua

Yapo mambo muhimu ambayo
yanapaswa kufanyika mara mama
mjamzito anapofikishwa kwenye
chumba cha kujifungulia.

Maumivu ya korodani (testicular pains)KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodani ili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo kubwa. Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na matatizo mbalimbali.

Madhara ya kunywa maji baridi:

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku.

Jinsi ya tunza afya yako

Kutunza afya yako kunaweza kuboresha utendaji wako shuleni, kazini na pia kuboresha maisha yako.
NI JAMBO linalopatana na akili kutunza mwili ambao Mungu alikupa. Kwa mfano: Wazia kwamba una gari, lakini hulitunzi. Muda si muda, gari hilo litaharibika. Jambo hilohilo linaweza kutukia kwa mwili wako.