Breaking News

September 30, 2013

Jinsi ya kutumia kondom za kiume na za kike kiufasaha

NUSU ya watu wanaotumia kondomu kwa ajili ya kujikinga na mimba ama magonjwa ya zinaa, hawajui namna ya kuitumia mipira hiyo

September 29, 2013

Tatizo la mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.

September 28, 2013

Chanjo ya safari kwenda nje ya Nchi

Kwa nyakati hizi ambapo milipuko ya magonjwa na sharia za uzuiaje wa magonjwa umefanya watu waweze kupatiwa kinga ya chanjo kabla hawajaenda Nchi Husika kulinga na uwezekano wa kuambukiza ama kuambikiza magonjwa huko waendako.

September 26, 2013

Jinsi ya kuzuia na kutibu kuharisha wakati unapokuwa safarini.

Kwa nini uharishe wakati ukiwa safirini?
Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika sehemu

September 25, 2013

Huu ndio ushuhuda wa mama huyu anayeishi na virusi vya ukimwi kwa miaka 25.
Pelegia Katunzi:Apambana na virusi vya Ukimwi
kwa miaka 25
Hii ni kutokana na ukweli kuwa, wakati huo
hazikuwepo dawa za kufubaza virusi vya
Ukimwi na kuchangia kasi ya kifo chake.
Pelegia anasema, wakati mume wake
anapimwa na kugundulika kuwa ana
maradhi hayo, alikuwa na ujauzito wa mtoto
wake wa mwisho. Naye alipimwa na
kugundulika kuwa ameathirika.
Uamuzi wa hospitali ukawa ni kumfanyia
upasuaji na kumtoa mtoto akiwa salama na
kumfunga kizazi.

September 24, 2013

Madhara ya chumvi


·         Stori kuhusu chumvi:
Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.

September 23, 2013

Jinsi ya kufanya tathimini ya hali ya lishe kwa mwili wako.

 1.1.   Chakula ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali .Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki.

September 22, 2013

Mambo muhimu kuhusu unyenyeshaji wa mtoto.

KATIKA zama hizi tunazoishi,
kumekuwepo na tabia ya baadhi ya
akina dada kukataa kunyonyesha
watoto wao kwa sababu hizi na zile.

September 21, 2013

Magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza,

Magonjwa makuu sita yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na: Ugonjwa wa kisukari, Magonjwa ya moyo, Shinikizo kubwa la damu, Saratani, Magonjwa ya figo na Magonjwa sugu ya njia ya hewa.

September 20, 2013

Jinsi ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za
kiume tunakuwa katika uwanja mpana
zaidi wa tafakari za kibaiolojia na
kisaikolojia walizonazo wanaume.

Madhara ya kiafya yasababishwayo na kufanya ngono kinyume na maumbile.

Ngono kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa nyia ya haja kubwa, ni hali ya kingono ambayo muhusika huingiza uume katika njia ya haja kubwa kwa lengo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujirishiza hisia zake.

September 19, 2013

Jinsi ya kujizuia usipate saratani ya matiti (breast cancer)

1. JICHUNGUZE MATITI YAKO.
Ukijichunguza mwenyewe mapema inasaidia
kugundua saratani mapema na kutibika kwa
urahisi, unatakiwa kujichunguza walau mara
moja kwa mwezi baada ya wiki moja ya
kwanza kupita baada ya hedhi,

September 18, 2013

Sababu 3 za mbu kutosambaza VVU/ UKIMWI


1. Kwanza mdomo wa mbu haupo kama
sindano za kawaida zinazotumika, mlija wa
mbu ambao hutumika kuingizia mate yenye
vimelea vya malaria ni tofauti na ule
unaotumika kufyonza damu kutoka kwa

September 17, 2013

Asali, asali!!!!!! Ni zaidi ya chakula

ASALI inafahamika kwa muda mrefu
kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na
magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee.

September 16, 2013

Ifahamu tofauti ya ugonjwa wa kaswende na kisonono

Ndugu msomaji nimeona ni muhimu kuandika tofauti ya ugonjwa wa kaswende na kisonono kwa sababu kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ambao wanapotoa maelezo

Uhusiano wa mazoezi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Ukweli utokanao na tafiti kuhusu umuhimu wa mazoezi katika
kujikinga na kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

September 14, 2013

Je, unaufahamu ugonjwa wa kifafa?

Kifafa ni ugonjwa wa ubongo
Ubongo wa binadamu una mabilioni yz seli za neva zinazoshirikiana na kila mmoja kupitisha chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima. Wakati baadhi ya hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na kusababisha kifafa ama kuzirai.

September 13, 2013

Jihadhari na kichaa cha mbwa (rabies)


Kichaa cha mbwa ni ugonjwa hatari sana unaowapata wanyama wote wanyonyeshao akiwemo mwanadamu na unapatikana nchi zote duniani isipokuwa katika bara la Antarctica.

September 12, 2013

Namna ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari.

 Ugonjwa huu hujulikana kitaalamu kama Diabetic Nephropathy.
Moja ya madhara ya ugonjwa wa kisukari katika mwili wa binadamu ni ugonjwa wa figo (diabetic nephropathy). Ugonjwa huu ambao huwapata watu

September 11, 2013

Mazoezi ni muhimu sana kwa afya ya binadamu

MAZOEZI ni muhumu sana kwa afya ya
binadamu lakini ni watu wachache sana
wenye nafasi au wenye kujua umuhimu wa
kufanya mazoezi ili kuujenga mwili pamoja
na akili.

September 9, 2013

Kabiliana na matatizo ya kiafya yanayoambatana na vvu/ukimwi kwa njia ya ulaji bora wa chakula.


Kuna matatizo mbali mbali ya kiafya yanayoambatana na VVU/UKIMWI. Matatizo
hayo yanaweza kuathiri mfumo mzima wa ulaji, umeng’enywaji wa chakula na
ufyonzwaji wa virutubisho mwilini. Baadhi ya matatizo hayo yanaweza kukabiliwa
kwa njia ya ulaji bora nayo ni pamoja na kuharisha,

September 8, 2013

Ugonjwa wa zinaa wa chlamydia

CHLAMYDIA NI NINI?
Chlamydia ni aina ya ugonjwa wa zinaa unaosababishwa
na bakteria aina ya chlamydia Trachomatis,
ambao wanaweza kuathiri viungo vya uzazi na pia kusababisha ugonjwa wa homa ya mapafu unaojulikana kama typical pneumonia.

September 7, 2013

Meningitis; uvimbe wa utandu wa ubongo na uti mgongo ni nini?

Huu ni ugonjwa unaothiri sehemu inayofunika ubongo na uti wa mgongo, yaani utandu. Ubongo unafunikwa na sehemu au tandu tatu nyembamba za seli ili kuitengenisha na fugu la kichwa. Tandu hizi zinaweza kuathirika na kusababisha hali inayojulikana kama uvimbe wa utandu wa ubongo na uti wa mgongo.

September 6, 2013

Huu ndio ugonjwa wa zinaa wa kaswende (syphilis)

Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum.  
Ugonjwa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.
Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana kama vile kujifungua kiumbe ambacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa,

Tatizo la mshituko wa moyo (heart attack) au myocardial infarction

Mshituko wa moyo kwa lugha ya tiba unajulikana kama 'Myocardial Infarction' inayomaanisha "Myo".. muscles au msuli, 'cardio'.... Heart au moyo na "infarct"....kufa kwa tishu kutokana na kukosa oksijeni

September 5, 2013

Sehemu ya pili: jihadhari na ulevi, haya ndio madhara na athari zake

ITAANZIA SEHEMU YA KWANZA
HII NI SEHEMU YA PILI NA MWISHO WA MAKALA HII KUHUSU ULEVI
Tulisema katika makala zetu zilizotangulia kwamba, utumiaji ulevi hupelekea kupatikana madhara mengi ya kimwili na kiroho kwa mtumiaji wa kinywaji hiki kilichoharamishwa.

September 4, 2013

Tatizo la shinikizo la damu (hypertension)

Shinikizo la damu au presha ambalo kitaalamu huitwa Hypertension au High Blood Pressure ni neno la kitiba linalotumika kueleza hali ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

September 3, 2013

Ugonjwa wa upungufu wa damu (anaemia)

Anaemia au upungufu wa damu ambao umekuwa tatizo kwa jamiii mbalimbali ulimwenguni, hususan katika nchi zetu za Kiafrika Tanzania ikiwa miongoni mwao.

Anaemia ni jina jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.

VIPI INATOKEA?
Upungufu huo wa damu hutokea iwapo ukolezi au mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu (haemoglobin) vinapopungua kupita kiwango cha kawaida.

September 2, 2013

Huu ndio ugonjwa wa kisukari au diabetes mellitus.


Ugonjwa wa kisukari au Diabetes Mellitus hutokea pale tezi kongosho au pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au  kitaalamu hyperglycemia.

September 1, 2013

Athari za sigara katika ugonjwa wa kisukari

Leo nazungumzia jinsi sigara, pombe,
vyakula na mfumo wa maisha wa mtu vinavyoweza kusababisha kisukari na kuleta madhara zaidi kwa mgonjwa wa kisukari,