July 30, 2013

Umuhimu wa kupima VVU kwa Wanandoa na wapenzi.


ONGEZEKO la maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa watu wengi linakua siku hadi siku. Na hii ni kutokana na watu kutoelewa umuhimu wa kupima VVU ili kujua hali ya afya zao kwa ujumla.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 65 ya watu waishio na VVU ni wanandoa wakati asilimia 35 ni vijana. Kutokana na takwimu hii wanandoa ni waathirika wakubwa wa janga hili hasa kutokana na kutokuwa waaminifu katika ndoa zao, haijalishi kama mwanamke au mwanaume mmojawapo anapotoka nje ya ndoa kuna hatari ya kupata maambukizi ya VVU. Maambukizi haya yanaongezeka kwa kasi hasa pale linapokuja suala zima la utegemezi wa kijinsia katika kupima VVU.

Idadi kubwa ya wanaume walioko katika ndoa hawako tayari kwenda kupima kwa hiari na badala yake kutegemea majibu yatakayopatikana kutoka kwa mama hasa wakati wa ujauzito hapa ndipo linapokuja suala la umuhimu wa kuyaelezea masuala ya usawa wa kijinsia na kutilia mkazo kwa wanandoa kwenda kupima kwa wakati mmoja.

Imefikia wakati wanandoa waone umuhimu wa kupima VVU kwa pamoja kwani itasaidia kuokoa maisha ya walio wengi na kupunguza kasi ya maambukizi hayo. Katika vituo vya kupima wajawazito, wanaume wanaokubali kuwasindikiza wake zao kupima kwa minajili ya kujua afya zao kiujumla ni wachache.

Na hata ukihoji sababu zinazowafanya waume hao kutohudhuria zahanati, utapewa majibu kuwa ni mihangaiko ya kukimbizana na maisha ndiyo inayowafanya wasihudhurie zahanati. Lakini ukweli ni kwamba wanaume hawako tayari na hawapendi kuwa karibu na huduma iliyoko katika vituo vya afya ili kujua afya zao.

Tunaweza kusema huu ni uoga wa wanaume kwani wanategemea kupata taarifa za upande mmoja, kwani mmoja kutokuwa na maambukizo ya VVU si kigezo cha mwingine kukosa maambukizi hayo.
Inawezekana kabisa kutokana na mfumo dume ulioko kwa wanaume walio wengi na dhana potofu walionayo kuwa kwao ni vigumu kupata maambukizi ya VVU.

Na hicho ndio chanzo cha maafa ya janga la ukimwi, vivyo hivyo idadi kubwa ya jamii ya Kitanzania bado haijapata elimu ya kutosha juu ya upimaji wa afya pamoja faida ya kupima mapema ili kujua afya zao.

Asilimia kubwa ya makundi yanayojitokeza kupima VVU ni wajawazito pamoja vijana walioko mashuleni. Kutokana na hilo wanaume bado ni tatizo katika upimaji wakati huo huo wao ndio wanaoongoza kuwa na mahusiano nje mbali na wake zao hii ni hatari, sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Inabidi Serikali kupitia wizara husika ingepanga mkakati wa kuanzisha kampeni ya kupima kwa hiari kwa kina baba, kampeni hii ingefanyika maofisini na kwingineko ingesaidia kuyapunguza maambukizi ya VVU.

Kutokana na taarifa na takwimu mbalimbali kutoka wizara ya Afya, wananchi wanaojitokeza kupima VVU, wanaume idadi yao ni ndogo.

Kupima kwa hiari kwa pamoja ni njia nzuri ya kupunguza maambukizi ya VVU hasa kwa wanandoa mfano pindi wazazi watakapojigundua tayari wamepata maambukizi wanaweza kuamua kutoendelea kuzaa tena ili kunusuru maisha ya mtoto au kama wataamua kuzaa basi watashauriwa kuzaa lakini kwa tahadhari ili kumlinda mtoto asipate maambukizi kwa kuanza kutumia dawa zitakazolinda mtoto asifikiwe na maambukizi hayo.

Pia kitendo hicho kitasaidia kuongeza upendo na uaminifu katika wanandoa. Usawa wa kijinsia katika kupima kwa wanandoa ni la kipekee katika mtazamo wa maambukizi ya VVU, 

Takwimu za awali zinaonyesha idadi kubwa ya waathirika ni wanandoa, wakati kundi linalofuatia ni vijana ambao hawajaingia katika ndoa. Upimaji wa ukimwi kwa pamoja kwa wanandoa utasaidia kuaminiana na kuongeza hali ya upendo katika ndoa. Hii pia itasaidia kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzie, hivyo hali hii hupunguza hata mahusiano ya nje kwa mwanaume au mwanamke.

Kwa kawaida kitendo cha kupima ni kigumu hata kwa watu walio nje ya ndoa hii hutokana kuogopa majibu yatakayotolewa kuwa huenda yakawa mabaya (yaani una maambukizi). Na hilo linatokana na kuwepo kwa rekodi mbaya ya mahusiano na watu mbalimbali, lakini kwa hali ilivyo sasa haiwezi kusababisha mtu kutopima.

Baba na mama mnapoenda kupima kwa pamoja na kujijua kuwa mmeathirika hatua zitakazofuata ni kupanga mikakati juu ya kuilinda familia yenu hasa watoto kabla muda wa kuishi haujaisha.
Hii ni nzuri tofauti na kukaa bila kupima ambapo watu huanza kutumia dawa za kuongeza siku wakati CD4 zimeshuka hivyo dawa kushindwa kufanya kazi mwilini na hatimaye mgonjwa kupoteza maisha wakati angeweza kusogeza siku za kuishi kwa kutumia dawa na kupanga mikakati juu ya familia.

Ndoa nyingi husambaratika sababu ya kupima kwa siri wapo wanaume wanaojigundua mapema kuwa wameathirika na hawako tayari kuwaeleza ukweli wake zao kuwa wameathirika na matokeo yake inabaki kuwa siri yake yeye mwenyewe kwa kuhofia kuachana na mwenza wake.

Usiri huo wa kuficha majibu ni hatari kwasababu unapomueleza mwenzio mapema inakuwa rahisi kwa ninyi kupunguza maambukizi na si kwamba kutasababisha ugomvi ndani ya nyumba.

Hata baadhi ya wanawake wajawazito wanapopimwa VVU na kukutwa na maambukizi huwa wanaficha na kufanya siri na matokeo yake baada ya kujifungua hafuati masharti ya kutomnyonyesha mtoto na kusababisha mtoto kupata maambukizi kutoka kwa mama.

Lakini endapo mama huyo asingefanya siri na kumueleza mumewe majibu aliyopata wangeshauriana na kufuta taratibu ili kumfanya mtoto asipate maambukizi kutoka kwa mama.

Wanaume na nawapa elimu hii juu ya upimaji kwa pamoja na wake zenu na tupunguze mfumo dume wa kutegemea majibu kutoka kwa mwanamke pekee.
Share:

July 23, 2013

July 21, 2013

July 20, 2013

July 13, 2013

July 11, 2013

Maana ya Kukoma kwa hedhi/ Menopause

Menopause (hedhi kukoma mfululizo kwa miezi sita au zaidi), ni hatua ya mwisho ya mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke; aghalabu kwa sababu ya utu uzima. Hii ni hatua inayotanguliwa na kipindi cha mpito chenye mabadiliko mengi kutoka katika mfumo unaotabirika wa kuona hedhi unaoambatana na tezi za uzazi (ovaries) kutoa angalau yai

Share:

July 9, 2013

July 4, 2013

Athari za kutoa mimba

“NISEME?” Aliniuliza binti mmoja, tena kwa
hofu kubwa wakati namhoji juu ya matatizo
yawapatayo baadhi ya wasichana
wanaodiriki kutoa mimba, hasa kienyeji,
Share: